Wednesday, January 4, 2012

MWILI WA BALOZI MHINA WAAGWA DAR, UMEZIKWA LEO KOROGWE TANGA!

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal akiongoza sala maalum ya kuombea marehemu mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina, kabla ya mwili huo kusafirishwa leo kwenda Korogwe kwa mazishi. Shughuli hiyo ilifanyika nyumbani kwa marehemu, Wazo, Dar es Salaam.

Vijana wakibeba jeneza lenye mwili wa Balozi Mhina ulipowasili nyumbani kwa marehemu, Wazo ukitolewa hospitali ya Lugalo.
Masheikh na Wanazuoni wakisoma kisomo maalum cha kmuombea marehemu Balozi Athumani Mhina.
          Wanafamilia wakiwa katika majozi wakati wa shughuli ya kusaifirishwa mwili wa marehemu.
Waziri Nchimbi akifarijiana na Naibu waziri wa Nishati na Madini Adamu Malima (kulia) na Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (katikati) kwenye msiba huo.

No comments:

Post a Comment