Thursday, August 18, 2011

KITUO CHA VIJANA SARAFIA CHAOMBA MSAADA WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA!

Mkuu wa kituo cha vijana kinacho jishughulisha na maadili mema kilichopo Bunju, Jijini DSM ABUBAKAR ZUBEIR ameiomba jamii kukisaidia kituo hicho kufuatia kukabiliwa na matatizo mbalimbali.

Mkuu huyo ametoa wito huo kwa ujumbe kutoka nchini Iran ulipotembelea kituo hicho ukiongozwa na Mkuu wa kituo cha utamaduni cha IRAN hapa nchini MORTEZA SABOURI.


Amesema kituo kwa sasa kinao jumla ya vijana wapatao mia sita kutoka mikoa mbali mbali huku kikiwa bado kinakabiliwa na matatizo mengi yakiwemo uhaba wa vitabu na vifaa vingine muhimu vinavyohitajika katika mafundisho.

No comments:

Post a Comment