Thursday, August 18, 2011

POLISI JIJINI YAKAMATA 55 KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI NA KUKUTWA NA SILAHA!

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya DSM limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 55 wa makosa mbalimbali ya uhalifu wakiwemo wa Ujambazi wa kutumia silaha pamoja na risasi 22.

Kutokana na Matukio hayo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SULEIMAN KOVA ametoa wito kwa askari binafsi kuwa makini pindi wanapokuwa katika malindo yao ikiwa ni pamoja na kuepuka kupewa vyakula ama vinywaji na watu wasiowatambua vyema.


Kamanda Kova pia amewataka Wamiliki wa Makampuni binafsi ya ulinzi hapa nchini, kutoa mafunzo na mbinu mbalimbali za kukabiliana na wahalifu kwa askari wake lengo likiwa ni kukomesha wizi ambao ni tishio kwa uchumi wa taifa.

No comments:

Post a Comment