ABDULKARIM HASSAN SHAH akiwa na Waziri Mkuu PINDA
Mawaziri nchini wametakiwa kutokubali kuwa mbuzi wa kafara kwa kukaa kimya mambo yanapoharibika na badala yake wawachukulie hatua za kisheria watendaji wanaowaangusha katika kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.
Akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi bungeni mjini Dodoma Mbunge wa Mafia (CCM) ABDULKARIM HASSAN SHAH amemuomba Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa OMARI NUNDU kuwakamata watendaji wote waliouza mali za Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA hadi watakapoeleza zilipo fedha za shiriko hilo.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa SHAH amemuomba Waziri NUNDU kuwashirikisha wabunge wa jiji la Dar es Salaam katika kulipatia ufumbuzi suala hilo kutokana na udanganyifu ulioanza kujitokeza.
No comments:
Post a Comment