Thursday, August 4, 2011

SHIRIKA LA AGAPE AIDS CONTROL LATOA SEMINA KWA WAFANYAKAZI WA NDANI!

SHIRILA lisilo la kiserikali la AGAPE AIDS CONTROL la mkoani Shinyanga leo limeendesha semina kwa watoto wanaofanya kazi majumbani lengo likiwa ni kuwapa watoto nafasi ili waweze kutoa sauti zao.

Mratibu wa shirika hilo John Mnyala amekiambia kituo hiki kwamba semina hiyo imeweza kukusanya watoto hao kutoka maeneo mbalimbali ya manispaa ya shinyanga na kuitaka jamii kuacha mara moja kuwanyima watoto haki zao za msingi.


Nae mmoja wa washiriki hao mtoto Amina Mdeka mwenye umri wa miaka 12, amebainisha kuwa katika uzoefu wake wa kazi za ndani amekutana na matatizo mengi ikiwemo kutaka kubakwa na baba mwenyenyumba.

No comments:

Post a Comment