Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetahadharisha kuwa Uganda pia inaelekea kukumbwa na baa la njaa ambalo linashuhudiwa hivi sasa katika nchi za Pembe ya Afrika.
Msemaji wa shirika la FAO amesema kuwa, kutokana na kuelekea kumalizika akiba ya chakula nchini Uganda, usalama wa chakula kwa taifa hilo upo hatarini na huenda wananchi wake wakapatwa na yale yanayoshuhudiwa hivi sasa katika nchi za Somalia, Kenya, Ethiopia na Djibouti.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema, zaidi ya maeneo 6 nchini Somalia yamo katika hatari ya kutokea janga la kibinadamu kutokana na ukame huku zaidi ya Wasomali milioni mbili wakikabiliwa na njaa.
Itakumbukwa kuwa, mwanzoni mwa mwezi Julai, takwimu za Umoja wa Mataifa zilibaini kuwa, hali ya mambo inazidi kuwa mbaya katika Pembe ya Afrika huku watu milioni 12.4 wakihitajia msaada wa dharura katiki nchi za Kenya, Ethiopia, Somalia na Djibouti.
No comments:
Post a Comment