Warembo 5 kati ya 30 wanaowania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, ambao wamefanikiwa kuingia fainali za kusaka taji la TOP MODEL wakiwa wamejipanga mbele ya majaji baada ya kufanikiwa kuingia katika hatua hiyo usiku wa Agosti 9,2011 katika Hotel ya Giraffe Ocean View jijini Dar es Salaam. Mshindi wa taji la TOP MODEL atajinyakulia tiketi ya moja kwa moja ya kuingia Nusu Fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011.
Majaji wa shindano hilo wakiumiza vichwa kutafuta mshindi. Warembo wote walikuwa wakati lakini 1 ndo anahitajika. Mshindi wa TOP MODEL anataraji kutangazwa leo katika siku maalum ya Waandishi Wa habari kufanya mahojiano na Washiriki hao wa Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe.
Washiriki wakipita mbele ya majaji
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania ambao hawakufanikiwa kuingia katika Fainali wakiwa wameketi.
No comments:
Post a Comment