Wednesday, August 10, 2011

WENYE DEPOT WAANZA KUUZA MAFUTA KWA WENYE VITUO VYA MAFUTA!

 
Baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA kutoa saa 24 kwa wamiliki wa Kampuni nne ambazo zilisitisha kutoa huduma za usambazaji mafuta kupinga kushushwa kwa bei ya bidhaa hiyo kampuni hizo zimeanza rasmi kugawa mafuta kwa wenye malori kama walivyoagizwa na serikali.

Uchunguzi uliofanywa na kituo hiki kwenye maghala ya kampuni hizo ambazo ni BP, ENGEN, OIL COM na CAMEL OIL yaliyoko Kurasini jijini Dar es Salam umeshushudia malori ya mafuta yakiingia kujaziwa mafuta tayari kwa kupelekwa kwenye vituo mbalimbali vya mafuta nchini.


Akizungumza bungeni mjini Dodoma Waziri wa Nishati na Madini WILLIAM NGELEJA alizitaka kampuni hizo kutii sheria za nchi na kuanza kutoa huduma hiyo mara moja badala ya kulumbana na serikali.


Serikali kupitia Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) tayari imeipa leseni kampuni tanzu ya shirika hilo COPEC kuanza kufanya biashara ya mafuta.

No comments:

Post a Comment