Thursday, August 4, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MABANDA MAADHIMISHO YA 18 NANE NANE DODOMA!

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo kuhusu matumizi ya moja ya kifaa cha Trekta linalotumika kwa matumizi ya Kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Tela la Trekta linalotengenezwa nchini, wakatiti wa wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijaribisha kuwasha Trekta la kilimo, baada ya kumkabidhi funguo ya Trekta hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Teresia Huvisa (kushoto) kwa ajili ya matumizi ya kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo Agosti 03, 2011 ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Bwigiri Wasioona, Achimpota Nicolaus na kumtazama mmoja wa wanafunzi wasioona, Hasanat Athuman, kuhusu jinsi wanavyowafundisha wanafunzi wasioona, wakati alipotembelea katika Banda la Wilaya ya Chamwino kwenye maonyesho maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa kutoka Kituo cha kudhibiti Panya Mkoa wa Morogoro, Eugen Ngolohela, kuhusu Panya aina ya Ndezi na wengineo, wakati alipotembelea katika mabanda ya maonyesho ya Maadhimisho ya Nane Nane leo Agost 03, 2011 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment