Muungano wa asasi za kiraia nchini zinatarajia kufanya maandamano ya amani katika siku ya kuadhimisha kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julisu Kambarage Nyerere Octoba 14 mwaka huu kwa ajili ya kuishinikiza serikali kutoilipa DOWANS tuzo ya shilingi bilioni 111.
Mkurugenzi wa asasi ya SIKIKA Bwana IRENEI KIRIA amewataka watanzania kuvaa nguo nyeusi katika siku kuadhimisha kifo hicho mpaka alipozikwa Octoba 23 kwa ajili ya kukumbuka msimamo wa Baba wa Taifa wa kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za taifa.
Nae Mkurugenzi wa chama cha waandiushi wa habari wanawake TAMWA Bi ANANILEA NKYA amesema hatua ya serikali kutaka kuilipa DOWANS inaonesha kuwa kuna baadhi ya viongozi wa serikali watanufaika na kugawana fedha hizo wakati mpaka leo wazee waliokuwa wafanyakazi wa jumuiya aya afrika mashariki pamoja na walimu bado wanaidai serikali mabilioni ya fedha.
No comments:
Post a Comment