Monday, October 24, 2011

JUMLA YA MIRADI KUMI YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 129.2 YAZINDULIWA NA MBIO ZA MWENGE DODOMA!

Jumla ya miradi kumi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 129.2, imezinduliwa pamoja na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru mwaka huu, Mkoani Dodoma. Mkuu wa mkoa huo, REHEMA NCHIMBI amebainisha hayo wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru, kwa uongozi wa mkoa wa Singida, yaliyofanyika katika kijiji cha Lusilile, wilayani Manyoni.

Amesema kuwa, miradi hiyo imegharamiwa na wananchi, serikali kuu,taasisi za fedha, wadau wa maendeleo, taasisi za hifadhi ya jamii pamoja na serikali za mitaa. Amebainisha kuwa miradi yote iliyofunguliwa, ukiwemo ule uliohusisha chuo kikuu cha Dodoma(UDOM),inaonyesha mafanikio yaliyopatikana kwa miaka 50 ya uhuru mkoani Dodoma.

Naye mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.PARSEKO KONE amesema ukiwa mkoani humo, Mwenge utakimbizwa kilomita 348.2,kuweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi 18, yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milion 448.7,kisha kukabidhiwa mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment