Wednesday, August 3, 2011

SERIKALI YA KENYA YACHUKUA HATUA ZA KUPAMBANA NA UKAME!

Ili kukabiliana na maafa ya ukame ulioikumba pembe ya Afrika, serikali ya Kenya imechukua hatua zenye ufanisi ambazo zimeifanya nchi hiyo ijiepushe na baa la njaa.

Makala ya gazeti la Nation la Kenya inasema, Mei 30 mwaka huu Rais Mwai Kibaki wa Kenya alitangaza kuwa maafa ya ukame ni janga la kitaifa, na alifuta ushuru wa kuagiza mahindi kutoka nje, hatua ambayo si kama tu imeongeza uagizaji wa mahindi kutoka nje, bali pia imehimiza kushuka kwa bei ya mahindi iliyopanda kwa mara moja tokea mwezi Desemba.

Hadi tarehe 14 Julai baraza la mawaziri la Kenya liliamua kutoa ridhaa uagizaji wa mahindi ya ubadilishaji geni kutoka nje, na kutoa msaada wa dharura wa shilingi bilioni 8 ili kuimarisha kazi za serikali katika kupambana na utapiamlo, usafirishaji wa maji na matibabu ya mifugo, na kuwapa chakula shuleni watoto wanaotoka kwenye familia zenye hali duni.

No comments:

Post a Comment