USIA NKHOMA
Hospitali ya Taifa Muhimbili.Ubalozi wa Afrika Kusini hapa nchini kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) wameshiriki kufanya usafi kwenye wadi ya watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa saratani Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na kutoa misaada mbalimbali.
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini, USIA NKHOMA Amesema wameshiriki katika usafi huo ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Rais Mstaafu wa Afrika kusini NELSON MANDELA, hii leo pamoja na kuwafariji watoto hao.
Kwa upande wake Daktari wa Kitengo cha Kansa, JANE KAIJAGE, amewataka watu binafsi pamoja na makampuni mbalimbali nchini kuwatembelea watoto hao na kubainisha kuwa hali hiyo huwafanya wafarijike zaidi.
No comments:
Post a Comment