Friday, August 5, 2011

KITENDO CHA SERIKALI KUTOFANYA MAAMUZI KITALIINGIZA TAIFA KWENYE MAAFA!

                                         DAVID KAFULILA (Kulia) akiwa na LUSINDE
Mbunge wa Kigoma Kusini DAVID KAFULILA amesema kuwa, kitendo cha serikali kutofanya maamuzi kinaweza kuliingiza taifa kwenye maafa makubwa kwa watendaji kutumia fursa hiyo kujilimbikizia mali umma.

Akizungumza Bungeni mjini Dodoma Mheshimiwa KAFULILA amesema kwa kuwa serikali imeshindwa kuzipatia ufumbuzi kero za muda mrefu ikiwemo ya Shirika la Ndege nchini ATCL viongozi wake walegevu waondolewe ili kupisha damu changa zitakazobadilisha mfumo wa utendaji.


Akijibu hoja za Wabunge, Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa OMARI NUNDU aliahidi kuzitumia shilingi Bilioni 95 zilizoongezwa na serikali kwenye bajeti yake kushughulikia kero mbalimbali zinazozikabili sekta ya reli, ndege na usafiri wa majini.

No comments:

Post a Comment