Friday, August 5, 2011

MAMA NKURUNZINZA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU SITA!

                DK. DENISE BUKUMI NKURUNZINZA akiwa na Mama SALMA KIKWETE
Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Burundi, DK. DENISE BUKUMI NKURUNZINZA amewasili nchini jana kwa ajili ya ziara ya siku sita kwa lengo la kujenga mahusiano ya karibu ya kidemokrasia baina ya mataifa hayo.

Akizungumzia ziara hiyo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini ( WAMA), MAMA SALMA KIKWETE, amesema kuwa mbali na kujenga mahusiano ya kidemokrasia pia ataangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tasisi hiyo.


Aidha kwa upande wake Dkt. DENISE BUKUMI NKURUNZINZA, amesema hana budi kuishukuru nchi ya Tanzania kufuatia kuwa moja ya mataifa yaliyotoa mchango mkubwa katika utatuzi wa mgogoro nchini humo ikiwa ni pamoja na kuwapa hifadhi Wakimbizi wa Burundi wakati wa machafuko nchini humo ambao miongoni mwao wamepewa uraia.

No comments:

Post a Comment