Tuesday, March 13, 2012

SERIKALI YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA HUDUMA ZA MACHO!

Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akizindua Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam ambapo Tanzania imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya Glaukoma duniani ambayo imeongozwa na kauli mbiu isemayo “Usiachie Glaukoma isababishe giza kwenye maisha Yako”

Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi Kaimu mganga mkuu wa Serikali Dkt. Donarld Mpando nakala ya Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho utakaoanza kutumika nchini mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi nakala ya Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini mwakilishi wa waandishi wa habari waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mkakati huo Bi. Zaina Jongo Malongo kutoka Gazeti la Mwananchi leo jijini Dar es salaam kufuatia umuhimu wa waandishi wa habari katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu sera mbalimbali.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Emmanuel Mhehwa(kulia) ambaye ni mlemavu wa macho juu ya namna anavyoweza kutumia kompyuta maalumu za watu wenye ulemamavu kuandika na kuhifadhi taarifa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.Taarifa za wizara ya afya na ustawi wa jamii zinaonyesha kuwa Tanzania ina watu karibu laki 450,000 wasioona na watu 1,350,000 wenye uoni hafifu.
 Msanii wa Muziki na Kiongozi wa Bendi ya Muziki ya Mjomba (Mjomba Band) Bw. Mrisho Mpoto (kushoto) akifikisha ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa macho na umuhimu wa kuwahi matibabu ya macho katika vituo vya afya ili kuzuia upofu leo katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akifurahia jambo na mwimbaji na mpiga gitaa mahili wa Bendi ya watu wenye ulemavu (Blind Beat Band) mzee Bonifasi Kiyenze leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini. Bandi hiyo ni miongoni mwa vikundi vya burudani vilivyoalikwa kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Vijana kutoka kikundi cha sarakasi cha Bandi ya Mjomba kikionyesha umahiri katika mitindo mbalimbali ya sarakasi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment