Friday, August 19, 2011

JUKWAA LA KATIBA TANZANIA LAZINDUA RASMI MWONGOZO WA KATIBA KWA RAIA!

                                          Mwanaharakati DEUS KIBAMBA (Kushoto)
Jukwaa la Katiba Tanzania limezindua rasmi mwongozo wa Katiba kwa raia ambao utakuwa mahususi katika kuelezea kwa ufundi na wepesi utaratibu, mchakato na masuala muhimu ya kuzingatia katika mchakakato wa kuandika katiba ya Kidemokrasia kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw DEUS KIBAMBA amesema mwongozo huo unatoa historia ya katiba ya sasa, mambo yaliyojiri na kusukuma upatikanaji wa katiba zote tano za nchi tangu uhuru pamoja na kupendekeza namna ya kuandika katiba mpya inyoendana na wakati.


Kwa msaada wa taasisi ya Policy Forum na wadau wengine tayari Jukwaa la Katiba Tanzania limeanza kusambaza bure nakala za kitabu hicho cha mwongozo lengo likiwa kuifikia jamii yote.

No comments:

Post a Comment