Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar DK ALLY MOHAMMED SHEIN amewataka wakulima na wafugaji nchini kushirikiana na kumaliza migogoro ya ardhi inayowakabili ili kudumisha umoja na amani iliyopo nchini.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya 18 ya Sikukuu ya wakulima maarufu Nanenane mkoani Dodoma DK SHEIN amesema, migogoro iliyopo baina ya wakulima na wafugaji isipomalizwa inaweza kuhatarisha usalama wa Taifa.
Kuhusiana na mkakati wa Kilimo kwanza Rais SHEIN aliwasisitiza wakulima nchini kujikita kwenye kilimo cha umwagiliaji ili wanufaike na nguvu kazi yao wanayoitumia.
No comments:
Post a Comment