Monday, August 8, 2011

WASHIRIKA WA STANBIC BENKI WAIKOPRESHA SERIKALI USD DOLA MILIONI 250!

Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa mkopo wa ushirika na Benki ya Stanbic wa dola za Kimarekani Milioni 250/- ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 375/- za Kitanzania utakaokuwa wa mikupuo mitatu ambapo fedha hizo zimekusanywa kutoka kwa wawekezaji wa ndani na nje.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba huo Waziri wa Fedha Mheshimiwa MUSTAFA MKULO amesema mkopo huo wa bei nafuu utatumika kuboresha miundombinu hususani ya reli ya kati na Tazara, barabara, umeme na usafiri wa majini.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic Bank Tanzania Bw.BASHIR AWALE amesema mkopo huo usiokuwa na masharti yoyote ni wa muda mrefu na wamefikia hatua hiyo kutokana na imani waliyonayo kwa Serikali ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment