Kocha Kondo Nassoro akimwelekeza bondia chipukizi Zainabu Mhamila (Ikota) uku nyuma akielekezwa jinsi ya kutembea na kocha Habibu Kinyogoli wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es Salaam.
KLABU za ngumi za ridhaa za Ashanti na Amana zimewataka vijana wenye vipaji vya mchezo huo kujitokeza kujiunga na klabu hizo ili kuendelezwa vipaji vyao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha mkuu wa Klabu ya Ashanti Rajab Mhamila 'Super D' alisema kutokana na kugundua kuwepo na vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza ngumi na kukosa watu wa kuwaendeleza hivyo wameona ni fursa pekee ya kuwachukua na kuwaendeleza katika Klabu zao.
Alisema, baada ya mkoa wa kimichezo wa Ilala kuanzisha mapambano ya kuhamasisha mchezo huo wameona vijana wengi waliokuwa na moyo wa kutaka kucheza mchezo huo hivyo wameona watoe nafasi kwa vijana hao kujiunga katika Klabu zao.
"Mimi na kocha wa Klabu ya Amana, Habibu Kinyogoli tumeamua kwa nia moja kuiwaendeleza vijana katika ngumi hizi hivyo tumeona tutoe nafasi kwa vijana wenye kipaji cha ngumi kujitokeza kujiunga na klabu zetu bila gharama zozote ikiwa ni kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao," alisema Super D.
Alisema, mabondi hao watapata nafasi ya kupambana ulingoni mbele ya mashabiki huku katika mafunzo wakiwa wananolewa na yeye akiwa pamoja na Kinyogoli na Kondo Nassoro ambapo wote ni makocha wa kambi ya mkoa wa Ilala. Aliongeza kuwa wakiwa ni waanzilishi wa ligi ya kuhamasisha ngumi hizo kwa mkoa wa Ilala na Dar es Salaam kwa ujumla wameamua kuendelea kupanua wigo huo kwa kuongeza idadi ya mabondia pia katika klabu zao. Picha kwa hisani ya Super D.
No comments:
Post a Comment