Thursday, March 8, 2012

TPBO YAMPONGEZA KOCHA WA NGUMI KIMATAIFA SUPER D!

Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa inakupa pongezi na shukrani nyingi kwako Rajabu Mhamnila 'Super D' kwa jinsi unavyoutendea haki mchezo wa ngumi za aina zote za kulipwa na za ridhaa.

Tunalazimika kutowa maneno mazuri na ya faraja kwako kwa kuwa umekuwa muhamasishaji mkubwa sana wa mchezo wetu huu ambao umetengwa na wadhamini lkn una wapenzi wengi tu katika nchi yetu ya Tanzania.

Umekuwa ni msaada mkubwa sana katika kila maandalizi ya mchezo kwa kuwasaidia waandaaji mapromota ambao hupungukwa vifaa vinavyohusu mchezo hususan glovus na kadhalika, pia umekuwa ukifuatilia mapambano ya ngumi popote pale hata mkoani ,na huku ukiripoti yote yanayofanyika huko ukiwa nje ya Dar es salaam kwa galama zako mwenyewe.


Hali kadhalika umekuwa ukiwasaidia mabondia wa mikoani kwa kuwauzia vifaa vya mchezo kwa bei ndogo kuliko hata ile ya madukani, hivyo kuwawezesha mabondia hao kuwa na uwezo wa kumiliki vifaa vya ngumi
kiurahisi.


Sisi TPBO.tunayo macho yenye kuona na kuthamini michango ya watu wa aina yako hivyo tunakuahidi kukupatia cheti cha kuthamini mchango wako katika tasnia hii ya mchezo wa ngumi , ktk wakati muafaka
utakapofika.

Pia ni kwa mwakilishi wa SHIRIKISHO LA NGUMI ZA KULIPWA [WORLD PROFESSIONAL BOXING FEDERATION LENYE MAKAO MAKUU NCHINI MAREKANI, NITAKUWA NIKIKUPATIA TAARIFA MUHIMU ZA JINSI GANI MABONDIA WA KULIPWA
WA TANZANIA WANAINGIZWA KWENYE VIWANGO VYA SHIRIKISHO HILI KUBWA,ILI WAWEZE KUPATA NAFASI YA KUGOMBEA MIKANDA YA SHIRIKISHO HILI KUBWA.


NINAAMBATANISHA KWAKO HATI YA UTEUZI WA KUWA MWAKILISHI WA SHIRIKISHO HILI ILIWATANZANIA WAHABARISHWE KUPITIA MTANDAO WAKO NA WASHIRIKA WAKO.


THANX IN ADVANCE
YASSIN ABDALLAH-USTAADH
RAIS -TPBO NA MWAKILISHI WA WPBF NCHIN TANZANIA.

No comments:

Post a Comment