Rais JAKAYA KIKWETE leo amefungua rasmi Maonesho ya 18 ya Sikukuu ya Wakulima ‘Nanenane’ mkoani Dodoma na kubainisha azma ya Serikali katika kusaidia sekta ya Kilimo, mifugo pamoja na uvuvi kwa kuyaongezea thamani mazao hayo katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akihutubia katika ufunguzi rasmi wa sherehe hizo rais kikwete amesema serikali itaendelea kuongeza fedha kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo za kilimo lengo likiwa ni kumkomboa mkulima, na akatoa wito kwa maafisa wa serikali kuacha vitendo vya kuwadhulumu wakulima haki zao.
No comments:
Post a Comment