Zaidi wa wahitimu 50 kutoka Taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini mwishoni mwa wiki walikusanyika makao makuu ya Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na kushiriki katika Siku ya Ajira iliyoandaliwa na kampuni hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TCC, Bi CAROLINE KAVISHE amesema shughuli hiyo maalumu ina lengo la kupata wahitimu wanaoweza kupitia programu ya mafunzo kwa wahitimu wapya kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu na kuajiriwa baadaye.
Programu hii ilianza miaka kumi iliyopita lakini mwaka 2008 ilibadilika kidogo na kuwa ya miaka miwili tofauti na miaka ya awali ambapo wahitimu walifanya mafunzo ya miezi mitatu tu.
No comments:
Post a Comment