Monday, July 11, 2011

WAJUMBE WA BODI YA UDHAMINI VODAFONE KUTEMBELEA TANZANIA!

LORD MICHAEL HASTINGS
                                                               ELIZABETH FILKIN
Wajumbe wawili wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza wanawasili nchini kesho kwa ajili ya ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo ya jamii inayofadhiliwa na Vodacom.

Wajumbe hao LORD MICHAEL HASTINGS na ELIZABETH FILKIN watakuwa na ziara ya siku saba kutembelea taasisi ya CCBRT na mradi wa kusaidia wanawake wajasiriamali MWEI.


Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania SALUM MWALIMU amesema wajumbe hao pia watatembelea maduka ya Vodacom M-PESA katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam pamoja na kutembelea makao ya Vodacom Tanzania yaliyopo eneo la Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment