Sunday, July 10, 2011

RAIS MWAI KIBAKI AZINDUA TOVUTI INAYOTOA DATA MUHIMU ZA SERIKALI!

Rais Mwai Kibaki wa Kenya amezindua tovuti ya kipekee ambayo inaifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara inayowawezesha raia wake kupata data muhimu za serikali katika intaneti.

Rais Kibaki amesema baada ya kuanzishwa tovuti hiyo, Wakenya sasa wanaweza kusoma data muhimu za serikali na kushiriki katika utekelezwaji wa katiba mpya na vile vile kuiwajibisha serikali.
Serikali ya Kenya imetoa idadi kubwa ya maelezo kama vile taarifa za idadi ya watu na matumizi ya fedha za serikali kitaifa na katika majimbo ili kuimarisha uwazi. Maelezo hayo yanapatikana katika tovuti ya wazi yenye anuani ya www.opendata.go.ke
Katika mfumo uliokuwepo huko nyuma kila aliyetaka data ambazo sasa ni wazi alilazimika kupata idhini kutoka wizara husika jambo ambalo lilikuwa gumu sana na wakati mwingine halikuwezekana. Mkuu wa Jumuiya ya Teknohama Kenya Alex Gakuru amesema kuzinduliwa tovuti hii ni mwisho wa mfumo wa 'siri kali' uliozuia takwimu za serikali kuwekwa wazi kwa umma.

No comments:

Post a Comment