Friday, July 22, 2011

PATA HABARI ZA JIJINI DSM KWA UFUPI!

MKAZI WA TANGA AIOMBA MAHAKAKAMA KUHARAKISHA UAMUZI WA KESI YAKE!
Mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Mama Eliza mkazi wa Bombo mkazi wa Tanga ameiomba mahakama mkoani Tanga kuharakisha utoaji wa maamuzi kuhusiana na kesi ya nyumba ambayo anadai kuimiliki na kasha kuamriwa kumpisha mtanzania mwenye asili ya kiasia, hali iliyosababisha aishi nje kwa kipindi kirefu.


MGOMBEA UBUNGE TEMEKE KWA TIKETI YA CUF AZUNGUMZIA UFISADI WIZARANI

Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF amesema kitendo cha katibu mkuu wa wizara ya nisharti na madini kuziandikia barua idara zote zilizopo chini ya wizara yake kuomba mchango wa kusaidia kupitisha bajeti ya wizara hiyo ni vitendo ambavyo vinaendelea katika wizara mbali mbali kwa kuwapa rushwa wabunge wa kamati za bunge ili wapitishe bajeti zao.

CHAMA CHA SAU CHAWATAMBULISHA VIONGOZI WAKE WAPYA!
Chama cha sauti ya Umma (SAU) kimefanya utambulisho wa viongozi wapya ngazi ya taifa baada ya kufanya mabadiliko katika Idara mbalimbali zikiwemo Idara ya Vijana, Idara ya Mambo ya nje, Idara ya Uenezi, Idara ya Propaganda, Idara ya katiba, Uratibu na sheria. ambapo Kamati kuu imefanya mabadiliko katika sekretarieti kuu ya SAU iliyofanyika July 16 Mwakahuu, baada ya viongozi wa awali kuachia nafasi zao ili kupisha mabadiliko ya kiutendaji.

BENKI YA POSTA YATOA MSAADA WA UJENZI WA SHULE YA MSINGI MAISAKA BABATI!
Benki ya posta imemkabidhi Mbunge wa Babati Mjini msaada wa shillingi milioni moja kwa ajiri ya matengenezo ya shule ya msingi Maisaka katika halmashauri ya manispaa ya Babati iliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea wilayani humo mapema mwezi April.

WAFANYAKAZI NEW FONTILES TECHNOLOGY (NFT) WAGOMA KUDAI MISHAHARA YAO!
Wafanyakazi wa kampuni ya NEW FONTILES TECHNOLOGY (NFT) inayojishuhulisha na promotion za matangazo ya makampuni ya simu leo wamegoma kufanya kazi hadi pale muajiri wao atakapowalipa mishahara yao pamoja na marupurupu wanayodai kwa zaidi ya miezi mitatu, huku uongozi wa kampuni hiyo ukishindwa kutoa maelezo juu ya tatizo hilo.

MSAMA AUCTION MART YAENDELEZ MSAKO DHIDI YA MAHARIMIA WA KAZI ZA WASANII
Kampuni ya Msama Auction Matt kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa kazi za wizi za wasanii pamoja na Mtambo unaotumika kuzalishia kazi feki za wasanii zipatazo 1, 382 zenye dhamani ya shilingi Milioni 11, Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Magomeni Usalama kwa maojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment