Friday, July 22, 2011

MISS ILALA WASAFIRI KWA ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI NA ZIWA MANYARA!

Warembo watakaoshirki mashindano ya kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya Ilala wameondoka kwenda Arusha na Nairobi kwa ziara ya siku nne ambayo ni safari ya kimafunzo na Utalii .

Leo wakiwa Nairobi, wanategemewa kukutana na Miss Kenya ambaye pia anashikiria taji la Dunia la Urembo wenye Malengo ( Miss World 2011- Beauty with Purpose). Mlimbwende huyo atawapa darasa kuhusu urembo wenye, malengo, kujiamini na kujua usichana ni nini. Pia wakiwa Nairobi, warembo watatembelea kambi ya Wasichana watakaoshiri kwenye shindano la kumtafuta Miss Kenya na kufanya nao mazungumzo. Watatembelea tembelea sehemu zenye kuvutia za mji huo na kurejea Arusha.


Warembo wanatarajia kutembelea mbuga ya Taifa ya Manyara kuona wanyama na kujifunza kuhusu urithi wa Taifa letu na baadaye kurejea mjini Arusha na kufanya shoo kwenye klabu ya Matongee.


Msafara wa warembo kumi na tano na unaongozwa na Afisa utamaduni wa Manispaa ya Ilala Mama Shani Kitogo anasaidiana na Afisa Habari Msaidizi wa Manispaa. Wengine katika Msafara huo ni Regina Joseph ambaye ni Mkuu wa Kambi, Bahati Chando- Matron, Adelhard Adex -Mkuu wa Itifaki na Nidhamu na Emma Mbangarara – Ulinzi na Usalama. Warembo wanaosafiri ni Maria John, Jenifer Kakolaki, Priscilla Mchemba, Nasra Salim, Diana John, Faizal Ali, Maryvine Kenzia, Godliver Mashamba, Edna Mnada, salha Israel, Augostina Mshanga, Lilian Paul, Mariam Mashamba na Ritha Joseph.


Safari ya kimafunzo ya kwenda arusha na Nairobi imewezeshwa na Vodacom Tanzania ambao pia wamewawezesha warembo kuendelea kuwasiliana na ndugu na jamaa kwa kuwapatia simu mpya na muda wa maongezi. Tofauti na mitandao mingine kadhaa ukiwa na line yako ya Vodacom unaweza kuendelea kuwasiliana na ndugu na jamaa ukiwa nchi yoyote na kwa warembo watakao kuwa Kenya wataweze hata kuongeza salio, kutuma ujumbe na kufaidika na kufaidika na huduma zitolewazo na Vodacom wakiwa nchini Kenya kupitia washirika wao ambao ni Safaricom.


Shindano la Miss Ilala linategemewa kufanyika Siku ya Vunja jungu, Ijumaa ya tarehe 29 Julai katika viwanja vya Mnazi mmoja katikati ya jiji la Dar es salaam.


Redds Miss Ilala 2011 imedhaminiwa na Redds original, Vodacom Tanzania, Paradise City Hotel, Paris Pub, Tanzania Standard newspapers, Jambo leo, Papazi Entertainment, Fabak Fashion, Channel Ten, TV Sibuka, Syscorp Group, 88.4 Clouds FM na B2C company.

No comments:

Post a Comment