Sunday, June 26, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.

Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakipita mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu suala zima la kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2011.

Baadhi ya vijana waliowahi kutumia madawa ya kulevya wakipita na mabango mbele ya jukwaa la mgeni ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yenye ujumbe wakitaka kusaidia dawa na Serikali dawa za kuzuia kutumia madawa, wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2011.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bertha Mamuya (katikati) wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, Juni 26, 2011, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2011.

No comments:

Post a Comment