Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Moshono mkoani Arusha wameiomba serikali kuharakisha mchakato wa kuwalipa fidia baada ya maeneo yao yaliyo karibu na Kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packers Limited kubadilishwa matumizi yake na kutengwa kwa ajili ya eneo la jeshi.
Akizungumza na kituo hiki Mmoja ya wakazi wa eneo hilo BI MARTHA TEMBA amesema, baada ya utathimini huo uliofanywa na Maofisa wa Ardhi walizuiwa kuyaendeleza makazi yao ikiwemo shughuli za kilimo ambapo ametumia fursa hiyo kuhoji atakayewajibika yatakapojitokeza maafa kama kulipuka kwa mabomu.
Kutokana na hilo wakazi hao wameiomba serikali kuliweka wazi jambo hilo kwani licha ya Mbunge ELISA MOLLEL ambaye amemaliza muda wake kulifikisha bungeni hadi sasa hawajapata mrejesho juu ya anayehusika kuwalipa fidia ili wahame.
No comments:
Post a Comment