Tuesday, May 10, 2011

MMYIKA- MATENGENEZO BARABARA YA MBEZI HADI MAKABE KUANZA!

                                                                     JOHN MNYIKA
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika amesema matengenezo maalum ya barabara ya Mbezi mpaka Makabe kupitia Lubokwe na mji mpya yataanza mwezi huu mara baada ya kupungua kwa mvua zinazoendelea hivi sasa.

Mnyika ameyasema hayo katika mkutano wa wananchi wa Mtaa wa Mbezi Luis uliofanyika katika eneo la Kona ya Miembesaba.
Amesema matengenezo hayo ambayo yanatarajia kugharimu takribani milioni 170 yametokana na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi wa Mbezi Makabe kuhusu ubovu wa barabara hiyo.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Barabara Mtaa wa Mbezi Luis, Samwel Kirama alimshukuru mbunge kwa kushiriki katika mkutano huo na kumweleza kwamba fedha kutoka mradi wa TASAF awamu ya pili kiasi cha shilingi milioni 28 zimeingizwa katika akaunti ya mradi kwa ajili ya ujenzi wa barabara nyingine katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment