Tuesday, May 10, 2011

WADAU WA KILIMO SHINYANGA WATAKA SERIKALI IWAWEZESHE KILIMO CHENYE TIJA!

Wadau wa Kilimo mkoani Shinyanga wakiwa kazini
                                             Hili ni moja ya Shamba mkoani Shinyanga

Wadau wa kilimo Mkoani Shinyanga wameitaka serikali kuweka mikakati itakayo wezesha kilimo nchi kuwa na tija badala ya ilivyo sasa kilimo kimekuwa na siasa zisizokwisha.
Hayo yameelezwa kwenye mdahalo wa maendeleo kuhusu kilimo kwanza uliofanyika katika ukumbi wa Ibanza manispaa ya shinyanga ambapo Mmoja wa wadau hao Bw George Katalama ameeleza kuwa Sera ya kilimo kwanza imemwacha mkulima na hivyo wakulima walio wengi hawaielewi.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Amina Masenza alikufungua mdahalo huo amesema kuwa mdahalo huo ufanyike kabla ya bajeti za halmashauri kupitishwa ili mawazo yanayotolewa yafanyiwe kazi kulingana na bajeti iliyopo.

No comments:

Post a Comment