Tuesday, June 21, 2011

BAADHI YA WAKIMBIZI WALIOREJESHWA MAKWAO WARUDI NCHINI KINYEMELA!

                                                  Baadhi ya wakimbizi wakirudi makwao.
                                    Mkimbizi akiwa katika kambi ya wakimbizi.
Serikali imekiri kwamba kuna idadi ya wakimbizi ambao walirudishwa makao lakini wakarejea nchini kinyume na Sheria ambao bado inawasaka ili hatimae iweze kuwarejesha tena makwao.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Shamsi vuai Nahodha amesema wizara yake kwa kushirikiana na kamati za ulinzi inafanya doria ili kuweza kuwabaini
Waziri nahodha amesema serikali imetoa uraia kwa wakimbizi wa Burundi 162,156 walioingia nchini mwaka 1972 na kwamba wakimbizi waliopewa uraia waliopo kwenye makambi ya katumba na mishamo bado hawajasambazwa katika mikoa mingine kama ambavyo serikali imekusudia.

No comments:

Post a Comment