Wednesday, October 12, 2011

OXFAM TANZANIA YAANDAA MKAKATI KUHAKIKISHA WANAWAKE VIONGOZI WANATEKELEZA MAJUMU YAO!


Shirika la Oxfam kupitia Mtandao wa Elimu Shinyanga SEN umeandaa mikakati ya kuhakikisha kuwa wanawake viongozi wanapata fursa ya kutekeleza majukumu yao ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo wa kujiamini wakati wa kutoa maamuzi sehemu zao za kazi.
Akizungumza kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na mtandao huo yaliyofanyika Manispaa ya Shinyanga Makamu mwenyekiti wa mtandao huo Tiluliundwa Sullus amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake viongozi hawajiamini sana kwenye kuoa maamuzi.


Wakati huo huo afisa mipango wilaya ya shinyanga vijijini Bi.MWAJABU ABDULLAH amesema kuwa kuendelea kuwa na viti maalum kwenye nafasi ya uongozi kwa wanawake ni kuendelea kuwadidimiza wanawake hivyo viti hivyo vifutwe ili kuwe na usawa wa kusimama majukwaani.

No comments:

Post a Comment