Monday, October 10, 2011

VODACOM FOUNDATION YAKABIDHI MADARASA MAWILI KWA SHULE YA SEKONDARI TAI RORYA!


Mkuu wa Wilaya ya Rorya Bw. Benedict Kitenga (kulia) akaikata utepe kufungua madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yaliyojengwa katika shule ya Sekondari TAI wilayani humo kwa msaada wa Vodacom Foundation, (kushoto) ni Meneja wa mfuko wa huduma za kijamii (Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule.
002: Meneja wa mfuko wa huduma za kijamii wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule (kulia) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yaliyojengwa kwa msaada wa mfuko huo katika Shule ya Sekondari TAI iliyoko Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, (kushoto) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Richard Okore.
Haya ndiyo madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yaliyojengwa na mfuko wa huduma za kijamii (Vodacom Foundation) katika Shule ya Sekondari ya TAI ilyopo Rorya Mkoani Mara ikiwa ni sehemu ya shuguli za mfuko huo kwa jamii.

No comments:

Post a Comment