Wednesday, October 12, 2011

MKAZI SINZA ALALAMIKIA KUNYANYASWA NA MGAMBO WA MANISPAA YA KINONDONI!

                                           Mwenyekiti wa Mtaa huo akifafanua jambo.
Mtu mmoja mkazi waSinza Jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la AGATHON PETER amelalamikia kunyanyaswa na mgambo wa Jiji wa Manispaa ya Kinondoni kwa kuporwa fedha zake kiasi cha shilingi elfu sabini, kufungwa pingu na kutozwa faini kubwa kinyume cha utaratibu.

Akizungumza na kituo hiki PETER amesema mwishoni mwa wiki iliyopita alikuwa anaongea na simu maeneo ya Magomeni Hospitali akakamatwa na mgambo wawili waliomfunga pingu mikononi wakidai kuwa alikuwa akijisaidia haja ndogo katika eneo hilo jambo ambalo anasema haikuwa kweli na baadae kumtoza faini ya shilingi elfu sitini.
Peter amesema baada ya tukio hilo alifanikiwa kufika polisi na kufungua kesi lakini baadae polisi walimkabidhi kwa mgambo hao ili akalipe kwanza faini kabla ya kuendelea na kesi yake ambayo alikuwa ameifungua ingawa awali mgambo hao walimpigia simu kumtaka wakutane ili wamlipe fedha zake.


Kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo SEBASTIAN MHOWERA amekiri mtu huyo kutozwa kiwango kikubwa cha faini na kusema kuwa anafuatilia suala hilo ili kuona kama stakabadhi zilizotumika niza Manispaa au zimeghushiwa. Kwa upande wa polisi Magomeni wamekiri kufunguliwa kwa kesi kituoni hapo na kusema kuwa wao siyo wasemaji wa polisi.

No comments:

Post a Comment