Thursday, October 6, 2011

MSAMARIA MWEMA ATOA FEDHA TASLIMU KWA MLEMAVU ILI AKAJIUNGE NA CHUO CHA MWALIMU NYERERE!

Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds Media Group Ltd BI JOYCE SHEBE akimkabidhi  kiasi cha fedha taslimu shilingi 800,000/- zilizotolewa na msamalia mwema kwa Mlemavu Frida Kavishe alizoomba kwa ajili ya kulipia ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi  katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Anayeshuhudia ni kaka wa Frida, Omari Mkete.
Msamaria mmoja jijini Dar es Salaam amejitokeza kumsaidia BI FRIDA KAVISHE ambaye ni Mlemavu wa mguu kwa kumpatia fedha taslimu shilingi 800,000/- ili akalipie ada ya masomo ya Shahada ya Uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni.



Msamaria huyo amekataa kutaja jina lake na kusema kuwa ameguswa na taarifa zilizotolewa na kituo hiki juu ya mlemavu huyo aliyepata nafasi ya kujiunga na chuo na kwamba ametoa ili BI FRIDA atumiea fursa yake ya kusomea masomo ya uchumi.


Akipokea msaada huo BI FRIDA amesema anamshukuru msamalia huyo kwa kutimiza ndoto zake na kuahidi kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa.


Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa CLOUDS MEDIA GROUP Mkuu wa Kitengo cha Habari BI JOYCE SHEBE amewaomba wasamaria wengine kuwa na moyo kama huo wa kusaidia makundi yak watu wenye uhitaji.

No comments:

Post a Comment