Monday, June 13, 2011

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO NEW YORK!

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake, Haji Hamis, akizungumza na kutoa utambulisho wa Viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo, wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipowatembelea wanajumuiya hao na kuzungumza nao jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake, wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo jana Juni 12, 2011.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na Vitongoji vyake ‘New York Tanzanian Community’ wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo jana juni 12.

No comments:

Post a Comment