Thursday, September 15, 2011

KAMATI MAALUM YA WANAWAKE DSM KUFANYA DUA KUWAOMBEA MAREHEMU WA MV SPICE ISLANDER!

                                                                      Bi. Zakhia Meghji
Kamati maalum ya wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa dua ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli iliyozama huko Nungwi Unguja- Zanzibar ambapo imewataka wanawake wa madhehebu yote kuhudhuria katika dua hiyo itakayofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini dar es salaam kesho jioni.

Akizungumza na kituo hiki, Mbunge wa kuteuliwa Bi. Zakhia Meghji ametoa wito pia kwa madereva, manahodha, na marubani wa vyombo vya usafiri hapa nchini kuhudhuria dua hilo.

No comments:

Post a Comment