Thursday, September 15, 2011

JESHI LA POLISI KITENGO CHA AFYA LAHAKIKISHA LINAPUNGUZA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YANAPUNGUA!

Jeshi la polisi kitengo cha Afya limesema limejipanga vyema katika kuhakikisha maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yanapungua ndani ya jeshi hilo kwa kutoa mafunzo yatakayo nuisha sera ya maboresho katika mitaala baada ya kuonekana mapungufu katika jeshi hilo.

Akizungumza katika semina iliyoratibiwa na Chama cha waandishi wa habari dhidi ya UKIMWI Tanzania AJAAT, kuhusu mkakati wa pili wa sera ya Ukimwi sehemu za kazi uliofanyika jijini Dar es salaam, Afisa Mnadhimu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, ACP BWELEKA ABIHUDI KILONZO amesema kwa kutumia tafiti, jeshi limebaini mapungufu katika mafunzo ambapo haki za binadamu, Jinsia na Ukimwi hayakupewa kipaumbele.


Aidha amevitaka vyombo vya Habari kutilia mkazo kwa kutoa taarifa ili jamii iweze kufahamu namna ya kujikinga na kuepuka maambukizi ya virusi vya ukimwi kazini.

No comments:

Post a Comment