Friday, August 26, 2011

SUMA JKT YAZINDUA PROMOSHENI YA KILIMO KWANZA KUELIMISHA WAKULIMA!

Wadau wa kilimo nchini wametakiwa kuhamasisha dhana ya kilimo kwanza nchini kwa kuhakikisha pembejeo za kilimo ikiwemo matrekta, mbolea, matrekta ya mkono, mbegu bora zinawafikia wakulima hususani walio katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi.

Akizindua promosheni ya Kilimo kwanza inayoendeshwa na SUMA JKT Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar DK HAFFAN OTHUMAN MAALIM amesema kama matrekta yaliyoingizwa nchini yangewafikia wakulima hali ya uzalishaji chakula ingeongezeka.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya SUMA JKT Meja Jenerali Mstaafu LIGATE SANDE amesema lengo la promosheni hiyo itakayotoa matrekta yenye thamani ya shilingi Milioni 99 kwa washindi ni kuwaelimisha wakulima kutumia shamba darasa na hatimaye kukifanya kilimo kuwa chenye tija.

No comments:

Post a Comment