Wednesday, October 5, 2011

MIKANDA YA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA TPBO YABAKIA MKOA WA TANGA!


Bondia Saidi Mundi wa Tanga (kushoto) akimwadhibu bondia Mohamedi Bakari wakati wa mpambano wao wa kugombea ubingwa wa uzito wa kilo.52 uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga jumamosi iliyopita, Mundi alishinda kwa T.K.O raundi ya pili na kuwa bingwa wa ngumi za kulipi TPBO.
Bondia Saidi Mundi wa Tanga akinoshwa mkono juu baada ya kumtwanga Mohamedi Bakari wakati wa mchezo wa kugombania mkanda wa ubingwa wa taifa wa chama cha ngumi za kulipwa TPBO viwanja vya tangamano TANGA.
Bondia, Alan Kamote wa Tanga akinyoshwa mkono juu na Refarii Yasina Abdalah baada ya kumshinda Yohana Robert wa Dar kwa pointi na kutawazwa kuwa bingwa wa kg.60 wa chama cha mchezo wa ngumi za kulipwa TPBO katika pambano lililochezwa viwanja vya tangamano tanga mwishoni mwa wiki.
Bondia Haji Juma wa Tanga akinyoshwa mkono juu na Refarii Yasina Abdalah baada ya kumtwanga bondia Juma Selemani na kutoa ubingwa wa ngumi za kulipwa TPBO katika viwanja vya tangamano mkoa wa tanga(picha na www.superdboxingcoach,blogspot.com).

No comments:

Post a Comment