Sunday, August 28, 2011

DK MIGIRO ALAANI SHAMBULIO LA KUJITOA MUHANGA OFISI ZA UN NIGERIA!

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dokta ASHA ROSE MIGIRO ameahidi kuimarisha hatua za kupiga vita ugaidi, kufuatia shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika makao makuu ya ofisi za umoja huo nchini Nigeria, lililosababisha vifo vya watu 19.

Dokta MIGIRO ametamka hayo mjini Abuja, wakati uchunguzi wa shambulio hilo ukiendelea kufanywa na polisi wa Nigeria na maafisa wa shirika la upelelezi la Marekani-FBI. Amesema wanalaani vikali shambulio hilo, lakini kitendo hicho cha ugaidi kitaimarisha dhima yao ya kupambana na ugaidi wa kila aina.


Dokta MIGIRO alietembelea makao makuu ya umoja huo yaliyoteketezwa katika mlipuko wa bomu na kusema kuwa hilo lilikuwa shambulio dhidi ya ubinadamu.

No comments:

Post a Comment