Friday, August 26, 2011

NCCR MAGEUZI KUVICHUKULIA HATUA VYOMBO VYA HABARI INAVYOKICHAFUA!

Chama cha NCCR – Mageuzi kimesema kitavichukulia hatua vyombo vya habari vinavyodaiwa kuandika taarifa za kichochezi dhidi ya chama hicho juu ya kuwepo kwa kikao kilichoketi kumjadili Mwenyekiti wa Chama hicho, Bwana JAMES MBATIA.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, SAMUEL RUHUZA, amekanusha kuwepo kwa kikao hicho na kudai kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote huku chama hicho kikiadhimia kuvifikisha kwenye baraza la habari vyombo vilivyoandika taarifa hizo.


RUHUZA ameongeza kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa Chama hicho kufungua kesi Mahakamani kupinga uchaguzi wa Jimbo la kawe ni haki yake ya msingi kutokana na mwenendo wa Uchaguzi huo ulivyokuwa.

No comments:

Post a Comment