Friday, August 26, 2011

RAIS KIKWETE KUSALI EID MSIKITI WA GADDAF DODOMA!

Rais JAKAYA KIKWETE anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika swala ya IDD EL FITRI ambayo kitaifa itafanyika mkoani DODOMA katika msikiti wa GADDAF mnamo tarehe 30 au 31 August mwaka huu , kutegemeana na muandamo wa mwezi.

Aidha swala hiyo ya IDD EL FITRI katika mkoa wa DSM inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya mnazi mmoja, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa rais DK. MOHAMED GHARIB BILAL ambayo pia itahudhuriwa na mabalozi na viongozi mbalimbali wa serikali.

Sheikh wa mkoa wa DSM ALHAD SALUM amesema BAKWATA inawapa mkono wa IDD na baraka watanzania wote, huku akiwaasa waislamu kuendelea kumcha Mwenyezi Mungu kama walivyofanya wakati wote wa mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na wasichana kuendelea kuvaa mavazi ya heshima.

Ujumbe wa mwaka huu wa EId-El Fitri ni “wazazi wawalee watoto wao kwa mujibu wa mafundisho ya kiislam”.

No comments:

Post a Comment