Friday, August 26, 2011

MKAZI WA MWANANYAMALA AOMBA MSAADA MTOTO WAKE APELEKWE MILEMBE!

Mkazi wa Mwananyamala Ujiji Jijini Dar es Salaam BI SALOME KASUMANI ameiomba Taasisi ya Ustawi wa Jamii nchini kumpa msaada wa dharula kwa kumpeleka mtoto wake mwenye ugonjwa wa akili hospitali ya Milembe Dodoma ili akapatiwe matibabu baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kumruhusu kwa madai kwamba amepona. LIDIA

Akizungumzia hali ya ugonjwa wa mwanae BI SALOME amesema kwamba amekuwa akimtishia maisha kwa kisu, kumfukuza nyumbani kwake kila anaposhindwa kumpa fedha za matumizi.


Kwa upande wake LIDYA NYONI ambaye ni mpangaji wa BI SALOME anazungumzia mateso na adha anayoipata mama huyo kutoka kwa mwanae ambaye ni mgonjwa wa akili.

No comments:

Post a Comment