Friday, August 26, 2011

ACTION AID LAANZISHA MRADI WA ELIMU JUMUISHI KWA JAMII ILI KUONGEZA IDADI YA WANAOANDIKISHWA!

SHIRIKA lisilo la kiserikali linalofanya kazi na vyama vya watu wenye ulemavu katika nchini 11 duniani ikiwemo Tanzania, Action on Disability and Development(ADD) limeanzisha mradi wa elimu jumuishi kwa jamii hiyo kwa lengo la kuongeza idadi ya watoto wanao andikishwa,kusoma na kumaliza shule wakiwa na matokeo mazuri yatakayowafanya kwenda sekondari.

Akizungumza na kituo hiki kuhusianana mradi huo Mkurugenzi wa ADD hapa nchini Sixbert Mbaya amesema kwamba mpango huo wa elimu jumuishi umeanzishwa kutokana na kuwepo kwa mazingira magumu na miundo mbinu isiyo rafiki kwa watu wenye ulemavu na hasa wakati huu ambapo watoto wengi wanahitajika kwenda shule kufuta ujinga.


Mbaya amesema mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka huu na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wanaharakati wa haki za binadamu,halmashauri za wilaya,mkoa na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA).

No comments:

Post a Comment