Monday, August 29, 2011

DALALY PETER KAFUMU AIDHINISHWA NA KAMATI KUU KUIWAKILISHA CCM UCHAGUZI IGUNGA!

Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi iliyokutana jana chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais JAKAYA KIKWETE imemtangaza DK DALALY KAFUMU kuwa mgombea Ubunge wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga kwa tiketi ya chama hicho.

Akitangaza maamuzi ya Kamati Kuu ya Taifa ya CCM Bw NAPE NNAUYE amesema katika kuhakikisha chama hicho kinashinda kiti hicho kampeni hizo zitafunguliwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.BENJAMIN MKAPA.


Kampeni hizo zitakazoendeshwa kwa njia ya helikopta kutokana na hali ya jiografia ya Igunga, zitakuwa chini ya mlezi wa chama hicho mkoa wa Tabora Mh MWIGULU NCHEMBA ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki.

No comments:

Post a Comment