Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kumchukulia hatua za Kidiplomasia Balozi wa Libya nchini kwa kitendo chake cha kupandisha bendera ya Serikali ya Braza la Waasi Libya TNC.
Wakizungumza katika mahojiano maalum na kituo hiki wakazi hao wamesema ingawa kila ubalozi nchini una utaratibu wake lakini suala la bendera linapingana na msimamo wa serikali wa kutolitambua baraza la waasi jambo linalomuondolea madaraka balozi huyo baada ya kukikuka kiapo chake cha awali kinachomtambua MUAMMAR GADDAFI.
Kutokana na hilo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh BERNARD MEMBE amesema watazungumza na balozi huyo ili kumpa msimamo wa serikali wakati wakisubiri kutangazwa kwa serikali mpya ya Libya.
No comments:
Post a Comment