Tuesday, November 15, 2011

MRADI WA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI WADOGO WANAWAKE MWEI WAINGIA MWANZA!


Mratibu wa mradi wa MWEI wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Mgongo Emmanuel akitoa mafunzo ya awali kwa wanawake wa Usagara Mkoani Mwanza kuhusiana na mradi huo utakaowapa fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi katika biashara za ndogondogo.
Kikundi cha wanawake kutoka Usagara Mkoani Mwanza wakipata maelekezo ya namna ya kutumia huduma ya M-pesa katika simu za mkononi kutoka kwa Mratibu wa mradi wa MWEI Bw. Mbuyu Ally unaoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ukiwa na lengo la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kuendeleza biashara zao ndogondogo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wakipata maelekezo ya kutumia huduma ya M-pesa kutoka kwa Mratibu wa mradi huo Bw. Mgongo Emmanuel wakati wa mafunzo hayo yenye kuwawezesha kujikwamua kiuchumi yakiendelea huko Usagara Mkoa wa Mwanza.
Mratibu wa mradi wa MWEI unaoendeshwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Bw. Mgongo Emmanuel (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha wanawake wa Usagara Mkoa wa Mwanza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo kuhusu mradi huo ambao pia utawawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia biashara za ndogo ndogo.

No comments:

Post a Comment