Thursday, June 16, 2011

MTANDAO WA KIGAIDI WA AL QAEDA WAMTANGAZA AYMAN AL ZAWAHIRI KUWA KIONGOZI WAO MPYA!

Mtandao wa kigaidi wa al Qaeda, umemtangaza Ayman al-Zawahiri kuwa ni kiongozi wao mpya, baada ya kuuawa kwa Osama bin Laden na kikosi maalumu cha jeshi cha Marekani mapema mwezi uliopita.

Tangazo hilo limetolewa katika mtandao wa itikadi kali za kiislamu. Zawahiri alikuwa kiongozi namba mbili wa al Qaeda kwa muda mrefu.
Katika taarifa iliyotolewa hii leo, mtandao huo pia umesema kwamba utaendelea na vita vyake vitakatifu dhidi ya Marekani na Israel.
Wakati huohuo, mahakama katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta imemhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani mfuasi wa kundi la wenye misimamo mikali ya kiislamu Abu Bakar Bashir baada ya kumtia hatiani na makosa ya ugaidi.

No comments:

Post a Comment